The House of Favourite Newspapers

UNYAMA: BABA wa SAID Auawa KIKATILI, Kisa Chake Kitakutoa Machozi – Video

NI mfululizo wa ukatili wa kutisha kati ya wakulima na wafugaji! Siku ya tarehe 26.03.2019 ambapo mtu mmoja afahamikaye kwa jina la Jisu Urembo Tuwa (70) mkazi wa kijiji cha Lukenge Wilayani Kibaha, ambaye ni baba wa Said Mrisho aliyetobolewa macho na Scorpion, amepoteza maisha baada ya kuchomwa mkuki mbavuni kufuatia mapigano baina ya wakulima na wafugaji.

 

Katika mapigano hayo, watu wanne (4) wamejeruhiwa akiwemo Afisa mtendaji wa kijji cha Lukenge Maximilian Mtobu (34) ambaye amepata majareha katika sehemu za uso na kuharibiwa kwa simu zake za Mkononi ambazo zilitumika kupigia picha mifugo ambayo ilikutwa kwenye lambo la maji ambalo hutumika kwa ajili ya matumizi ya kijamii.

 

Akiongea na Global TV Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Abuu Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo lake na kutoa wito kwa wananchi kuepuka vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na akawaasa kuwa watulivu kipindi hiki ambacho jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwabaini na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika.

Comments are closed.