The House of Favourite Newspapers

Updates: Mbunge ‘Bwege’ Aachiwa kwa Dhamana

MBUNGE wa Jimbo la Kilwa Kusini kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Seleman Bungara anapenda kujiita ‘Bwege’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali kutoka jeshi hilo.

 

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amesema Bungara alikamatwa jana Jumatatu saa 10 jioni eneo la Maalim Seif lililopo Kilwa Kivinje.

Aidha, Ngubiagi amesema mbali na Bungara, wengine wanaoshikiliwa na polisi ni madiwani wanne akiwemo Diwani wa Kilwa Masoko na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka.

UPDATES:

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara ‘Bwege’ aliyekuwa anashikiliwa na polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali ameachiwa huru baada ya kukamilisha dhamana.

Video: Msanii Ampa Makavu Wema Sepetu

Comments are closed.