The House of Favourite Newspapers

Urusi Yaituhumu Ujerumani Kuwa ‘Kimbelembele’

0

IKULU ya Urusi, Kremlin, imewatuhumu madaktari wa Kijerumani kuwa na ‘kimbelembele’, baada ya kusema kuwa vipimo alivyofanyiwa kiongozi wa upinzani wa Urusi, Alexei Navalny, vinaonyesha alilishwa sumu.

 

Urusi imedai madaktari wa Urusi walimfanyia vipimo sawa na vya wenzao wa Ujerumani, lakini hawakugundua kilichomsibu.

 

Madaktari wa Siberia walisema Navalny, ambaye amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, amekumbwa na matatizo ya mwili wake kutofanya kazi vyema (metabolism), hali iliyosababisha apelekwe kwa matibabu huko Berlin, Ujerumani.

 

Muda mfupi baada ya Navalny kufikishwa Berlin,  madaktari walitangaza kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa alikuwa amesumishwa.

Leave A Reply