The House of Favourite Newspapers

Ushoga, Uchafu wa Diamond na Nandy, Mwakyembe Afunguka – Video

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota, Diamond Platinumz, ambaye tayari amekamatwa na polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.

 

Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi kumsaka msanii, Nandy ili naye ahojiwe kutokana na tuhuma kama hizo ambapo yeye video yake na Bil Nas ilisambaa mitandaoni wakijiachia kimahaba.

 

Mwakyembe amesema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyehoji akitaka kujua serikali ina mkakati gani kutokana na wimbi la wasanii kuachia video na picha zao utupu mitandaoni.

 

Aidha, Mwakyembe alisema Tanzania siyo kokoro la uchafu na kueleza kwamba wanaangalia taratibu za kuwafikisha Diamond na Nandy mahakamani kutokana na tuhuma hizo.

 

MSIKIE MWAKYEMBE AKIFUNGUKA

Comments are closed.