The House of Favourite Newspapers

Spika Amjibu Mbowe Kunyimwa Gari, ‘Kufutwa Upinzani Bungeni’ – Video

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametolea ufafanuzi hoja iliyotolewa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kuhusu iwapo kambi ya upinzani Bungeni imegutwa, huku akianika kuhusu kiongozi Mkuu wa kambi hiyo, Freeman Mbowe kunyimwa gari na serikali.

 

Ndugai amesema gari ya Mbowe ipo isipokuwa dereva aliyetakiwa kuliendesha gari hilo anatakiwa kustaafu hivyo wanafanya utaratibu wa kumtafutia dereva mwingine.

 

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa uongozi wa Bunge hilo umeamua watumishi wote wa vyama vya siasa Bungeni wasiwepo hivyo sio wa upinzania tu, hata wa CCM tayari wameondolewa, hivyo kambi hiyo kuendelea kugoma kuleta hotuba kwa kisingizio cha kutokuwa na mtu wa kuwaaandikia ni sawa na kujishusha hadhi.

MSIKIE NDUGAI AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.