The House of Favourite Newspapers

Usiku wa ya kale ni dhahabu… Bendi kongwe za Taarab kutikisa Dar Live

0

Stori: Andrew Carlos

BENDI kongwe za Muziki wa Taarab zikiwemo TOT, Zanzibar Modern, Muungano na nyingine kibao zinatarajiwa kukutana pamoja Mei 2, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Uwazi ShowBiz, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa tukio hilo litakuwa la kihistoria katika Muziki wa Taarab nchini.

“Kutakuwa na wakali wote wakiwemo Mzee Yusuf, Bi Mwanahawa, Patricia Hilary, Khadija Kopa, Joha Kassim, Ally Star, Misambano, Thabit Abdul, Bi Afua na wengine kibao na niwaambie tu itakuwa shoo ya kihistoria nchini,” alisema Mbizo.

Bendi za Taarab zitakazokuwepo ni pamoja na Babloom, Egyptian, All Stars, East African Melody, Jahazi Modern, JKT na Zanzibar Modern.

Leave A Reply