The House of Favourite Newspapers

Wanaume wa Dar bana… unajua mabegi haya yanabeba nini?

0

GABRIEL NG’OSHA NA SIFAEL PAUL
Wanaume wa Dar bana! Miongoni mwa maswali yanayoulizwa na wengi ni muonekano wa baadhi ya wanaume wa Dar wakiwa na mabegi migongoni. Kama ilivyo kwa wanawake ambao huwa na mapochi kwapani au mkononi, ukikatiza kona mbalimbali jijini Dar, huwezi kupitisha nusu saa bila kuona kijana au hata mtu mzima akiwa na begi mgongoni. Swali ni je, ndani ya mabegi hayo hubeba nini?
Over Ze weekend limeingia mzigoni kutafuta jibu la swali hilo kwa kuzunguka sehemu mbalimbali za Dar ikiwemo Posta, Buguruni, Temeke, Tabata, Mwananyamala, Makumbusho, Mbezi, Mwenge, Kariakoo, Tegeta, Kimara na kwingineko kuchunguza baadhi ya vijana kuhusu ukweli wa wao kubeba mabegi hayo mgongoni.

WAJASIRI-AMALI
Wao hubeba bidhaa kama saa, cheni, viatu, nguo, enka za kutundikia nguo, madela, bra na nguo nyingine kutokana na biashara husika.
WAPAKA RANGI
Wao hubeba baadhi ya vifaa ambavyo huvitumia katika kuwasafishia wateja wao ikiwemo, removal, rangi za kucha, kisugulio cha kucha

vinginevyo.

WANAFUNZI
Hubeba laptop, kalamu, vifaa vya kuchorea, madaftari, rim paper, vitabu, head phones na wengine body spray.

WAFANYAKAZI
Hubeba laptop, flash, power bank, ipad, kalamu, notebooks, plan paper, makabrasha ya ofisini, vitabu, miwani na vinginevyo vya kikazi.

MASHAROBARO
Hawa mara nyingi ni vijana ambao wako kwenye umri kati ya miaka 18 hadi 25. Kubeba begi kwao ni swaga, ndani yake kuna flash, memory cards, cd, vifaa vya gemu, body spray, head phones, walkman au deki mbovu ambayo inafanana na laptop ili naye aonekane amebeba laptop.
VIBAKA

Hubeba bisibisi, plaizi, spana, kisu kidogo cha kukunja, viroba, sigara, bangi na vinginevyo. Hivi huwa ni vitendea kazi katika matukio ya uporaji wa simu, mikoba ya akina mama, wizi wa bodaboda na vifaa

Leave A Reply