The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-9

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
“Mimi simuelewi Aisha…”
“Kwa lipi tena baby?” aliuliza Bony kwa mshangao mkubwa huku akihisi tayari limesanuka…
JIACHIE PEKE YAKO…


Kwani kama ni taa ilikuwa mbovu kwa nini asilale akasubiri kesho? Na anaposema ilikuwa asome, kwani lazima asome? Huu ni usumbufu mkubwa kwenye familia za watu. Kama anataka kuishi hapa inabidi afuate sheria zetu, vinginevyo nitakuwa simuelewi,” Neema alimwambia mume wake.
“Lakini hata mimi dear sikujisikia vizuri…”

“Ee! Umeona? Wewe ni mume wa mtu, kuingia chumbani kwake halafu usiku si sahihi.
Kama vile, nimeingia kuna giza, sasa maana yake nini? Je, mfano nigekuwa sipo, narudi nawakuta kwenye giza vile mume wangu, si ningefikiria vibaya?”
“Sana mke wangu.”
“Mimi sijapenda. Inaonekana kuna siku anaweza akaja kukutaka mume wangu…”
“Aaa wapi!”

“Aaa wapi nini? Yaani hawezi kukutaka au?”
“Siwezi kumkubalia.”
“Weee! Weee! Usinidanganye mimi…”
“Kweli sweet.”
“Apia…”

“Mungu vile,” alisema Bony huku moyoni akisema…
“Hakuna ubaya kuapa, kwani si amesema kuna siku anaweza kunitaka wakati sisi tumeshatakana.”
Neema alinyamazia hapo, hakuendelea kusema, lakini kwa uelewa wa Bony alijua mkewe amekasirika sana kwani si mtu wa manenomaneno kama wanawake wengine.

Lakini kwa kupitia kauli hiyo ya mume wake sasa, moyoni aliwaza…
“Kama hivi tu amemaindi na aliniruhusu mwenyewe, itakuaje siku akigundua natembea naye? Lazima patawaka moto na huenda damu itamwagika.”
***
Asubuhi iliyofuata, Jumatatu. Wote walitoka kwenda makazini huku, Neema akiwa si mwenye raha sana kama wakati mwingine hali ambayo, hata Aisha aliisoma.
Alipofika kazini kwake, Aisha alimpigia simu Bony…
“Sweet,” alisema Aisha…

“Yes darling,” alipokea Bony…
“Leo nimemwona Neema kama si mchangamfu, kuna nini au umemfanya nini?” aliuliza Aisha…
“Ah! Siku hazilingani, lakini mimi mbona nimemwona yuko sawasawa!”
“Mmmh! Basi kumbe humjui vizuri mke wako mwenyewe. Hayuko sawa. Mimi mpaka nilitaka kumuuliza.”

“Hamna bwana, yuko sawasawa na wala usiwe na wasiwasi,” Bony alimtuliza Aisha kiaina huku ukweli akiujua kwamba ni kuhusu tukio la jana usiku mwenzake amemaindi.
“Oke! Sasa darling ina maana leo ukitoka kazini ni moja kwa moja nyumbani au?”
“Yes baby, kwani vipi?”

“Hata, nimeuliza tu…mimi nilitaka tukakae mahali nikupe ofa hata kama ni nyama choma au mchemsho wa kuku.”
“Mahali kama wapi baby?” Bony aliuliza huku moyoni akiwa ameshaikubali ofa hiyo…
“Popote pale utakapopaona patatusitiri na macho ya watu wanaokujua wewe ni mume wa Neema.”
“Oke, basi Challenge Class nahisi panafaa.”
“Ni wapi?”
“Mbezi Beach.”
“Sawa.”

Waliagana kwa makubaliano ya kuendelea kuchati kwa meseji kila pale itakapotokea, mmoja anammisi mwenzake.
***
Saa kumi na nusu, Bony alimpigia simu Neema kumwambia anakwenda Mabibo kwa rafiki yake anaumwa hivyo atachelewa kurudi nyumbani…
“Poa baby,” alikubali Neema.
Nusu saa mbele, Aisha naye akampigia simu Neema…
“Shoga, natoka kazini lakini napitia kule nyumbani mara moja, kuna vitu nakwenda kuvichukua,” alisema Aisha…

“Sawa, lakini si hutachelewa?”
“Sitachelewa shoga.”

Bony aliendesha gari, akampitia Aisha mahali, wakaenda Challenge Class.
Walishuka wote, wakawa wanaingia huku wameshikana mikono na kutafuta mahali pa kukaa…
“Shemeji Bony,” aliita Nancy ambaye kwenye ndoa ya Bony na Neema yeye alikuwa matroni…
Bony aliachia mkono wa Aisha haraka sana…

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.

Leave A Reply