The House of Favourite Newspapers

Usipotoa Risiti ya EFD Faini Tsh Mil 4.5, Usipodai Faini Tsh Mil 1.5 – Video

0

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kuwasisitiza wafanyabiashara wanaotakiwa kutoa risiti za kielektroniki (EFD) wanapouza bidhaa ama kutoa huduma watoe risiti hizo kwa mujibu wa sheria na wananchi wanaponunua bidhaa ama kupokea huduma wadai risiti kwani kutofanya hivyo ni kuidhulumu Serikali mapato yake.

 

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Desemba 15, 2021 na Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi (TRA), Richard Kayombo wakati akizungumza mambo mbalimbali yahusuyo ulipaji kodi kupitia Kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio.

 

“Kama ulitakiwa ulipe kodi Desemba 31, lakini ikafika mwaka unaofuata Januari 1 hujalipa, madhara yake utapigwa adhabu na riba. Kwa nini usubiri riba na adhabu? Ndio maana tunawashauri kulipa kodi kwa wakati.

 

“Desemba ni mwezi muhimu kwa ukusanyaji kodi kwa sababu hii ni awamu ya mwisho ya mwaka, pia tunahamasisha watu kulipa mwezi huo kwa sababu ni mwezi wenye sikukuu, wengine wanakwenda likizo, na makampuni mengi mwaka wao wanafunga Desemba.

 

“Mifumo ya kielektroniki imetusaidia sana kupunguza usumbufu wa kulipa kodi,kwa sasa mfumo unamrahisishia mlipakodi kulipa kwa wakati na kupata taarifa papo hapo na pesa hiyo inakwenda Mfuko Mkuu wa Serikali moja kwa moja na kuirahisishia Serikali kupanga matumizi.

 

“Kwa waliokadiriwa walipe kodi mapema wasisubiri Januari kuna majukumu mengine, wanaouza bidhaa na wanatakiwa kutoa risiti za EFD watoe, wasipofanya hivyo adhabu yake ni kubwa (Tsh mil 3 hadi mil 4.5).

 

“Mwananchi ukinunua bidhaa dai risiti, usipodai risiti unaidhulumu nchi yako mwenyewe, ukikutwa umenunua bidhaa na hujadai risiti adhabu yake ni Tsh 30,000 hadi Tsh mil 1.5,” amesema Kayombo.

 

Leave A Reply