Usyk Ampiga Anthony Joshua

BONDIA wa Ukraine Oleksander Usyk (34) ameshinda pambano la Ubingwa wa Dunia uzito wa juu (heavyweight)  na kutwaa mikanda ya WBA, WBO, IBF na IBO kwa kumpiga kwa pointi bondia Anthony Joshua (31) wa England katika pambano la raundi ya  12 lilochezwa katika uwanja wa Tottenham London England, usiku wa kuamkia leo.

 

Majaji wote watatu walimpa Usyk ushindi kwa  pointi 117-112, 116-112, 115-113 , baada ya kichapo hicho Joshua amepoteza mikanda yote minne aliyokuwa anaishikilia.

 

Pambano hili lilikuwa la 19 kwa Usyk, 13 akishinda kwa KO huku akiwa hajawahi kupoteza hata pambano moja.

 

Joshua alipanga amtafute Tyson Fury ili wazichape kugombania mkanda wa WBC ambao ni wa uzito wa juu lakini mambo yamebadilika sasa hana mkanda hata mmoja.

 

Ikumbukwe kuwa Anthony Joshua ndiye mwanadamu pekee aliyewahi beba mikanda minne ya Uzito wa Cruise Weight ndani ya mapambano 15 tu.


Toa comment