The House of Favourite Newspapers

Utata Kifo Kigogo Bima

0

UTATA umeibuka kufuatia kifo cha Ofisa wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) mkoa wa Tabora aliyefahamika kwa jina la Yonami Ngabano Kimaro ambaye alikutwa amefariki chumbani kwake Januari 2, mwaka huu.

 

Kimaro ambaye alikuwa anaishi katika Kata ya Kidongo Chekundu – Tabora mjini kifo chake kimeibua sintofahamu kwa wakati wa kata hiyo.

 

Akizungumza na wananchi katika eneo la tukio, Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilayani Tabora, SSP Jackson Lema alisema polisi watafanyia uchunguzi kifo hicho.

 

Mara baada ya UWAZI kufika katika eneo la tukio lilishuhudia Polisi wakiuchukua mwili wa marehemu huyo kwa ajili ya kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete pamoja na kuufanyia uchunguzi.

 

Aidha, Lema aliwataka wananchi kusaidiana na Jeshi la Polisi hususani yanapotokea matukio ya uhalifu na yanayohatarisha maisha ya watu na mali.

 

Alisema marehemu alikuwa akiishi katika chumba alichokuwa amepanga kwenye mtaa huo wa Mkunazini alikokuwa akiishi peke yake huku familia yake ikidaiwa kuishi Arusha.

STORI: ABDALLAH AMIR, TABORA

Leave A Reply