The House of Favourite Newspapers

Utawala wa miaka 30 wa Al Bashir wa Sudan wang’olewa!

 

BAADA ya maandamano makubwa ya wiki kadhaa nchini Sudan yaliyokuwa yakimtaka Rais Omar Al Bashir kujiuzulu, habari zisizothibitishwa zinasema rais huyo ameng’olewa madarakani baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 30.

 

Habari hizo zinasema kinachofanyika sasa ni kuundwa kwa baraza la muda la kuiongoza nchi hiyo.

 

Taarifa za serikali zimesema leo kwamba  jeshi litatoa tangazo muhimu kuhusu hali ilivyo nchini humo.

 

Shirika la habari la Reuters limesema maelfu ya watu walifurika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi wakipinga makelele ya “Utawala umeng’oka, tumeshinda!”

 

Bashir ambaye nchi za Magharibi zilikuwa zinamtafuta kuhusiana na mauaji ya Darfur nchini Sudan, ameitawala nchi hiyo kwa muda mrefu zaidi ya kiongozi mwingine nchini humo tangu ilivyopata uhuru mwaka 1956.

 

Kama ni kweli ameng’oka, Bashir atakuwa ni kiongozi wa pili katika eneo hilo la Afrika kuondolewa madarakani baada ya aliyekuwa Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, kuong’olewa katika maandamano dhidi yake.

Comments are closed.