The House of Favourite Newspapers

Waziri Kama Unaweza ‘Kaivute Bangi’ ya Njombe – Video

Rais Dkt Magufuli ahitimisha ziara yake ya mkoa wa Njombe kwa kuhutubia maelfu wa wananchi uwanja wa Polisi Makambako leo Alhamisi Aprili 11, 2019 ambapo atafungua barabara ya Mafinga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7 katika eneo la Mtewele.

 

“Barabara hii ilikuwa imefikia mahali pabaya ilikuwa inasababisha ajali nyingi lakini pia ilikuwa nyembamba na magari yalikuwa ni mengi, barabara hii ni ni muhimu sana sio tu kwa Makambako bali kwa Tanzania nzima. Kukamilika kwa barabara hii kutachochea shughuli za kiuchumi lakini pia nina imani wakazi wa Njombe mtatumia barabara hii kupitishia mazao yenu kwenda mikoa mingine na hata nje ya nchi.

 

““Benki ya dunia wametukopesha hizi fedha tunazotakiwa kulipa na tumeshaanza kuzilipa hivyo hauwezi kumkopesha mtu ambaye unajua hawezi kukurudishia lakini sisi tumekuwa walipaji wazuri. Hatuwezi kukopa kwaajili ya chai ya Rais, Hatuwezi kukopa kwaajili ya Kulipa mishahara ya watumishi, Tunakopa kwaajili ya Miradi ya maendeleo ya wananchi wetu tunao watumikia hakuna nchi iliyoendelea ambayo haijakopa.

 

 

“Hatuwezi kukopa kwaajili ya mishahara, semina na kongamano wala kwa ajili ya mimi kusafiri kwenda nje bali tunakopa kwaajili ya miradi ya kusaidia wananchi wa chini, hata sisi tunapokopa hapa malipo yake hatutayamaliza kwenye awamu ya tano inaweza ikalipwa hata awamu ya kumi lakini barabara zitaendelea kujengwa ili tuweze kukuza uchumi wa nchi, hakuna nchi yoyote ambayo haikopi hata Marekani wanakopa.

 

“Tangu nimeingia Njombe nimeona nyumba zilizojengwa ni tofauti na nyumba za huko kwetu kwani zote ni za bati na zimejengwa kwa matofali ya kuchoma ninafikiri mikoa mingine ambayo haijabadilika katika ujenzi wa nyumba waje wajifunze huku.

 

“Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavuta bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta ili mradi wananchi wa makambako wapate maji. Ukimbembeleza sana mtoto wakati wa kula anaweza akadeka zaidi, Hebu mnase Kibao uone kama hatokula haraka haraka huo uji, wakati mwingine hatupaswi kubembelezana lazima tutumie nguvu ili mambo yaende. 

 

“Nilitoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo ili wasisumbuliwe lakini jana mlisikia kule ulambo mtu amekamatwa amechapisha vitambulisho vyake mwenyewe anauza vijijini na amepelekwa mahakamani,” amesema Magufuli.

Comments are closed.