The House of Favourite Newspapers

UTI; gonjwa linalosumbua wanawake -3

0

uti-lgTunaendelea kuchambua ugonjwa wa UTI. Matatizo ya maambukizi ya UTI licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo wa kike kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani. Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao huweza kupata maambukizi ya UTI iwapo watajisafisha kwa kutumia maji yasiyo salama ambapo huwa rahisi kwa bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia (govi).
Pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi ya UTI kutokana na sababu tuliyoitaja juu na ndiyo maana tohara kwa wanaume husisitizwa.

Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo husababishwa zaidi na bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kwa kuingia na kujikita katika mfumo wa mkojo.
Bakteria wengine wanaoleta maabukizo katika njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, trimonas na fangasi ambapo huwaathiri watu pale wanapojamiiana bila kutumia kinga na watu wenye maradhi hayo.

Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara ni vyema kutumia kinga na kwa mwanamke wanashauri kila wanapomaliza kufanya tendo la ndoa wakojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia. Baada ya kujua hayo yote hivi sasa tuzijadili dalili za ugonjwa wa UTI.
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali ijapokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo.

Dalili nyingine za UTI ni maumivu, kutokwa na usaha wakati wa kukojoa, kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati mkojo ukitoka.
Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wanapojisaidia haja kubwa. Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.

Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu, kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili huonesha kuchoka.

Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi. Matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona kabla huwapata watu wote wanawake na wanaume.
Watu wenye matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.

Wiki ijayo, tiba yake usikose nakala ya gazeti hili.
Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni. Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha madhara mengine kama vile shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji kazi mbovu wa figo.

Leave A Reply