The House of Favourite Newspapers

UVCCM Mkoa wa Dar Watakiwa Kusimamia Misingi ya Chama

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala akizungumza jambo katika kikao hicho. 
Kikao cha UVCC Mkoa wa Dar es Salaam kikiendelea.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Said Rusilawe akizungumza jambo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Said Rusilawe amewataka vijana wa jumuiya ya vijana Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia misingi ya jumuiya hiyo kwani ndiyo nguzo kuu ya chama inayozalisha viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi Katika ukumbi wa Anatouglou jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa baraza la vijana wa UVCCM la utekelezaji. Akielezea misingi ya chama hicho amesema UVCCM ni nguzo kuu inayopaswa kuzingatiwa katika mustakabali wa taifa
 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala amesema kuwa baraza lake lilifanya ziara ya kutembelea kila wilaya za mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kukagua fedha zinazotolewa na serikali kwa kila halmashauri za vijana kwa ajili ya mikopo ili kuweza kujishughulisha katika kuleta maendeleo.
NA DENIS MTIMA/GPL.

Comments are closed.