The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Msami anapenda tu kampani yangu

0

BAADA ya hivi karibuni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Msami kueleza kuwa hawajawahi kuachana kimapenzi, msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya ameibuka na kupinga vikali kauli hiyo. Akizungumza na Amani, Uwoya alisema hadhani kama mwanamuziki huyo alimaanisha hawajaachana kimapenzi, bali ni kwenye kuzoeana au kukutana na kupiga naye stori lakini siyo kuhusiana na mapenzi kama wengi walivyodhani.

“Nafikiri Msami alizungumzia kuhusu ukaribu wetu wa siku zote, lakini sidhani kama ni ishu ya mapenzi na kama ni ukweli wala asingezungumzia hivyo hadharani. Kikubwa ni kwamba Msami anapenda tu kampani yangu,” alisema Uwoya.

Stori: Imelda Mtema

Leave A Reply