The House of Favourite Newspapers

UWOYA: SIPENDI KUOGA, NAPENDA SANA POMBE!

0

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii pendwa ya My Style! Kama ilivyo kawaida, huwa tunakuletea mastaa wakubwa hapa Bongo na kuzungumzia maisha yao halisi hususan urembo, mitindo na maisha yao ya nyumbani.

Leo tunaye Irene Uwoya ambaye safu hii ilimtembelea nyumbani kwake ushuani, Masaki jijini Dar.

Mrembo huyo amefunguka mambo mengi usiyoyajua:

My Style: Uwoya awali ya yote, hebu tupe ratiba yako ikoje pindi unapoamka kila uchwao hapa nyumbani!

Uwoya: Nikiamka jambo la kwanza kufanya ni kusali, kisha baada ya hapo nitazunguka nyumba nzima ‘ku-refresh mind’ kisha nikimaliza nitakula mchemsho wa kuku kwa sababu ndio kitu ninachokipenda. Baada ya hapo nitaswaki, kisha naendelea na mambo mengine…

My Style: Jambo gani ambalo hupendi kabisa kulifanya?

Uwoya: Kitu ambacho sikipendi maishani mwangu ni kuoga, aisee sipendi hicho kitu balaa.

My Style: Jambo gani ambalo huwa unapenda sana kulifanya?

Uwoya: Napenda kwenda sehemu za watu ambao hawana uwezo, kukaa nao kubadilishana mawazo na kuwasaidia pale ninapoweza.

My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

Uwoya: Mimi starehe yangu kubwa ni kunywa, napenda sana kunywa pombe. Lakini starehe yangu nyingine ni kuangalia muvi.

My Style: Ukiwa na msongo wa mawazo, huwa unapenda kufanya nini au kwenda sehemu gani ambayo unahisi ndio utakuwa sawa?

Uwoya: Nikiwa na mawazo hakuna kitu nakifanya kama kula, maana naweza nikala hata mara tano kwa siku.

My Style: Viwanja vyako vikubwa vya starehe kwa hapa Bongo ni vipi?

Uwoya: Mara nyingi nikihitaji kutoka, huwa naenda kwenye baa yangu pale Last Minutes na kama sipo hapo, basi huwa napenda kuchukua boti nakuzunguka nayo kwa sababu mimi napenda sana maji, yaani asilimia 90 ya maisha yangu huwa naimalizaga kwenye maji.

My Style: Ukiwa unatoka kwenda kwenye event yoyote, juu mpaka chini huwa unatumia kama bei gani hivi?

Uwoya: Kiukweli mara nyingi huwa sipendi sana kuzungumzia kiasi gani cha pesa ambacho huwa nakitumia kwenye mavazi yangu.

My Style: Wewe ni chizi nini? (Kitu gani ambacho unakipenda sana).

Uwoya: Mimi ni chizi viatu na nywele, ukiingia chumbani kwangu utaona jinsi nilivyo na viatu vingi, maana kuna vingine nilinunua mpaka leo hii vina muda mrefu sijawahi kuvivaa.

My style: Kiasi gani cha pesa huwezi kukitoa kununua viatu hata kama unavipenda sana?

Uwoya: Mimi hata nikikuta kiatu kinauzwa Shilingi Milioni 10 kama nina hela nanunua, navipenda sana.

My Style: Kuna kipindi ulikuwa una tabia ya kuuza nywele ulizotumia (mawigi) hilo zoezi liliishia wapi?

Uwoya: Tena sasa hivi zimejaa, hivi nilikuwa nina mpango wa kumwambia dada wangu tunazifanyaje maana zimeshajaa na sina sehemu ya kuzipeleka. Kwa hiyo nataka tuzipeleke sokoni tena.

Uwoya: Rangi gani za nguo ambazo unazipenda sana?

My Style: Napenda rangi nyeupe na rangi ya njano.

My Style: Aina gani ya nguo ukiivaa unajiona uko comfortable zaidi na unajiona umependeza kuliko ukivaa nguo nyingine?

Uwoya: Nguo fupi kwa kweli, nikivaa nguo ndefu naona kama nawashwa yaani.

My Style: Unaweza kutoka bila make up?

Uwoya: Ndio, tena siku hizi mara nyingi huwa nafanya hivyo.

My Style: Asilimia kubwa ya wanaume huwa hawapendi wanawake wanaopenda sana kupaka make up, unahisi ni kwa nini?

Uwoya: Nahisi ni kwa sababu wanataka kuona uhalisia wa mtu, unajua saa zingine make up nazo zinachanganya unaweza kumuona mtu yupo hivi kumbe ni kituko. Kwa hiyo ni vyema ukamzoesha mpenzi wako sura yako halisi, ili hata baadaye ukipaka make up anakuwa ameshakujua ukoje, kwa hiyo mimi nahisi natural ina raha yake sana.

My Style: Unapenda kutoka na mpenzi wako akiwa katika muonekano upi wa mavazi?

Uwoya: Napenda avae pensi, raba, T-shirt yaani awe simpo. Sipendi masutisuti.

My Style: Unatembelea gari ya aina gani na gari ya ndoto yako ni ipi?

Uwoya: Kiukweli sina utaratibu mzuri kwenye magari, leo mashetani yangu yakinipanda nitatembelea gari na siku nyingine nakuwa sijisikii tu kutembelea gari hivyo naita Uber, lakini gari ya ndoto yangu ni Bugatti.

My Style: Unapendelea chakula na kinywaji cha aina gani?

Uwoya: Napenda makande na kinywaji changu pendwa ni pombe basi.

My Style: Msanii gani hapa Bongo ambaye mapigo yake yanakuvutia zaidi?

Uwoya: (Anacheka) Mimi mwenyewe kwa kweli, napenda sana ninavyovaa.

My Style: Kati ya saa, hereni na pete ni kitu gani ambacho huwezi kutoka bila kuwa nacho?

Uwoya: Saa, yaani hata nikifika mbali vipi lazima nitarudi kuichukua na cheni kwa sababu huwa siitoagi mwilini.

My Style: Irene ni mtu wa aina gani kwa ambao wamezoea kukuona tu kwenye tv?

Uwoya: Huwezi amini, mimi mwenyewe hata sijielewi ni wa aina gani maana hata walionizunguka pia hawanielewagi, yaani mimi ni sometimes yes sometimes no.

My Style: Kama sio kuigiza, kitu gani kingine ambacho ulitamani sana kukifanya?

Uwoya: Nilikuwa napenda sana kuimba sema sauti ndio sina.

My Style: Asante sana kwa muda wako.

Uwoya: Karibu tena.

MAKALA: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply