The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Aliyepona Akili Amweleza Lukuvi Alivyodhulumiwa Nyumba

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  akiongea na Ramadhan Sudi Balega.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  amemrejeshea mkazi wa Kigogo, Dar es Salaam, Ramadhani Sudi Balega, nyumba yake aliyodhulumiwa na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Macha.

 

Lukuvu alifanya hivyo alipozuru maeneo ya Kigogo na Msimbazi Centre jijini Dar es Salaami ambako alimrejeshea mtu huyo hati zake halali za kiwanja hicho chenye nyumba aliyokuwa ameanza kuijenga.

 

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mgogoro ulidumu kwa zaidi ya miaka kumi kutokana na  hila zilizosababisha kubadili hati kutoka kwa Balega kwenda kwa Macha.

 

‘’Nataka kuwapa matumaini wananchi wote walioonewa, haki yako itachelewa tu lakini ipo siku utarudishiwa haki yako.  Nataka kuwapa onyo watu wote ambao wanafikiri wanaweza kunyan’ganya haki ya masikini yeyote halafu serikali isiwaone; watambuwe kwamba serikali ipo macho na inashughulikia migogoro yote,’’ alisema Lukuvi akiwataka  wananchi kutoa ushirikianao kwa kuripoti matapeli na wadanganyifu wote waliyomo ndani au nje ya serikali.

 

Pia, Lukuvi alitembelea eneo la Msimbazi Centre lenye mgogoro wa muda mrefu kati ya Kanisa Katoliki na mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria, Harod Exavel,  ambapo eneo hilo limeonekana kuwa na hati mbili ambapo ile ya kanisa ilitolewa mwaka 1965.

 

Hali hii inatokana na watendaji wa Halmashauri ya Ilala kupitia moja ya vikao vyake kufanya makosa na kumpa hati  Huwell ambapo mwaka 2009, Huwell alimuuzia mmiliki wa Victoria eneo ambalo tayari wizara ilishafuta hati hiyo.

 

Lukuvi alifafanua kuwa  kwa mujibu wa sheria ni kosa kumilikisha hati juu ya hati nyingine au mchoro wa upimaji juu ya mchoro mwingine na kama ikitokea kufanya hivyo ni lazima yule mwenye hati ya awali arurudishiwe kwani kuna fomu maalumu ya serikali ( surrender form) inayojazwa kumwezesha  mtu kuingia kwenye ardhi yenye hati kuipima na kuipangia matumizi.

 

Hata hivyo,  Lukuvi amewataka wahusika, Kanisa Katoliki na mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria, kukutana naye  siku ya Ijumaa Septemba 2, 2019, saa tano asubuhi ofisini kwake Ilala Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna bora ya kutatua mgogoro huo.

Comments are closed.