The House of Favourite Newspapers

Video: Chimbuko La Bongo Fleva Kwenye ‘Old Is Gold’ | Global Radio

0

KIPINDI cha Bongo 255 kinachoruka kupitia Global Radio, Mei 14, 2020 kimepiga stori na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Jembe, kuhusu chimbuko la Bongo Fleva.

Amenukuliwa akisema  kukosa umoja baina ya wasanii wa Bongo Fleva kulisababisha muziki huo kushuka, ambapo wasanii wa Hip Hop na wale wa kuimba waliingia kwenye mgogoro kwa muda wa miaka miwili, juu ya ipi iitwe Bongo Fleva na ipi iitwe Hip Hop.


Waliingia kwenye mtafaruku mkubwa kiasi cha kupeana majina, kwamba wale wanaoimba wakaitwa wabana pua, na wale wengine wakaitwa watu ambao muziki wao hauuziki.

Aliyoyasema  Saleh Jembe  wakati wa kipindi:-

“Wasanii wa zamani wana haki ya kukata tamaa, wamepigana sana kwa muda mrefu kuufikisha huu muziki hapa ulipo, zamani wakati sisi tuna-rap tulikuwa tunatembea na tape, tulipambana ndiyo maana unaona wasanii wa sasa wanaweza kupata fedha, lakini wasanii wa zamani hawapati hiyo thamani,

 

“Kukosa umoja baina ya wasanii wa Bongo Fleva kulisababisha muziki huo kushuka, wasanii wa Hip Hop na wa kuimba waliingia kwenye mgogoro kwa muda wa miaka miwili, juu ya ipi iitwe Bongo Fleva na ipi iitwe Hip Hop.  Waliingia kwenye mtafaruku mkubwa sana kiasi cha kupeana majina, wale wanaoimbwa wakaitwa wabana pua, na wale wengine wakaitwa watu ambao muziki wao hauuziki,”

 

“Wasanii hawataki kusema ukweli, ila hii ilichangia sana kuushusha thamani muziki, kwa sababu baadaye wakawagawa mashabiki, wengine wakasema hatuwezi kuwasikiliza wabana pua na wengine wakasema hatuwezi kusikiliza muziki wa wahuni.

 

“Profesa Jay niliwahi kula naye mihogo wakati huo akiwa anaupambania muziki wa Bongo Fleva ufike hapa ulipo leo, jamaa katoka kwa Master Jay kurekodi, akaingia kwa Mama Ntilie kujipoza,

 

“Mimi nilikuwa namuombea Chid Benz apone na arudi kwenye gemu, yule jamaa anajua sana.  Anajua kuchana, anajua maana ya muziki wa Hip Hop, nafikiri yule akirudi akiwa stable, anaweza akaonyesha thamani ya Hip Hop na kuwafufua hawa wasanii wa zamani ambao wapo chini kwa sasa,

 

“Ukiwa unakua, ukimuona mtu mzima, unaweza ukahisi aliibuka na kuwa mtu mzima, kumbe siyo kweli kuna mambo mengi sana amepitia kwenye ujana, mimi pia nilikuwa na mawazo kama hayo.

 

“Watu wengi hawajui kuwa Eric Shigongo alikuwa DJ huko kwao Mwanza, alikuwa anajiita DJ Shigi, nilikuwa na picha yake moja amevua shati ameachia six packs, alikuwa ana-hustle, alikuwa anapita kijiji hadi kijiji kupiga muziki, mnaweza mkamwita siku moja akawapa stori nyingi kuhusu muziki, leo ukimuona kwenye korido unaweza ukahisi hajui vesi hata moja,

 

“Mimi nimefanya kazi na Marehemu Ruge, alikuwa anaupigania sana huu muziki wa rap, lakini tukaja kupishana na yeye baadaye, ambapo naye alikuwa anaamini kuwa Hip Hop siyo muziki wa biashara, mimi nikapishana naye hapo kwa sababu kwa upande wangu nilikuwa naamini tofauti,

 

“Ruge alimbadilisha Lady Jaydee, alikuwa ana-rap akaambiwa aimbe, kweli akawa anaimba, wakati huo Jaydee alikuwa anamiliki gari aina ya Vitara, alikuwa anatembea na tape recorders, alikuwa akikumbuka vesi anasimamisha gari, halafu anarekodi ili asisahau.

 

“Ruge alimwambia Dogo Ditto aache ku-rap kama ambavyo alikuwa anafanya na kina Afande Sele, akakubali baadaye akawa anaimba ndiyo zikaja hizo nyimbo kama Moyo Sukuma Damu.

 

“Shigongo alikuwa ni mwana Hip Hop na ndiye mtu pekee aliyeanzisha shindano kubwa la ku-rap wakati akiwa anaiongoza hii Global Publishers.   Shindano la Mfalme wa Rhymes, ambalo alishinda Afande Sele na akapewa zawadi ya gari ya kufunuka juu. Mpaka leo halijawahi kutokea shindano kama hilo.

 

“Kukosekana kwa mitandao wakati wa zamani, ndiyo chanzo cha wasanii wakongwe kutofanya biashara ya muziki kwa wakati huo.  Wasanii wa siku hizi wanavuna fedha kila sehemu na kwa urahisi sana.”

Leave A Reply