The House of Favourite Newspapers

Haji Manara Akiri Kuachana na Mkewe; ‘Nikasikia Ameolewa’

0

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema  ameachana na mkewe na tayari ameshaolewa kutokana na presha kubwa kutoka kwa familia ya upande wa mke wake.

 

Manara amesema kuwa ana mpango wa kuoa mke mwingine ambaye atakuwa mzuri huku suala la tabia akiliweka kando kidogo.

 

“Kulikuwa kuna presha kubwa sana upande wa mke wangu hadi nikafikia kuamua kuachana naye.  Siku chache baadaye nikasikia ameolewa, wala sikushtuka kwa kuwa hili nilijua lilikuwa limeandaliwa na linakwenda kuwa hivi.

 

“Kwa sasa nasubiri kwanza, lakini nitaoa, na mwanamke ninayetaka kumuoa lazima awe mrembo sana. Nataka mwanamke mrembo hasa, suala la tabia litafuatia,” alisema.

SHEHENA ya SUKARI Yatua Arumeru, Sasa Mambo Safi!

Leave A Reply