Sabby Angel: Mapenzi Yameniponza

MUIGIZAJImahili wa Bongo Muvi, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa mapenzi ya ulaghai yamempotezea dira ya maisha yake.

 

Akizungumza na Amani alisema, katika maisha yake ya kimapenzi alikutana na wanaume wengi ambao hawakuwa na mapenzi ya ukweli bali walipanga kumtumia na kumuacha.

 

“Unajua wanaume ndiyo mara nyingi huchangia kuharibu maisha ya wanamke, kama mimi nilikutana na wanaume wengi lakini wote hawakuwa sahihi kwangu.

 

“Kuna wengine walikuja na gia ya ndoa lakini baada ya muda mfupi waliniacha njia panda,” alisema Sabby Angel

Stori: Imelda Mtema


Toa comment