The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Hashim Rungwe Aomba Kukutana na Rais Magufuli Amshauri

0

Mwenyekiti wa Chama Cha Umma (Chauma), Hashim Rungwe amesema ingefaa Rais Dk. John Magufuli akawaalika viongozi wa siasa ili waweze kumpa ushauri wa kiuchumi na kisiasa ili nchi iweze kupiga hatua kimaendeleo.

Akizungumza na Global TV hivi karibuni, Rungwe alisema kuna mambo ya msingi ambayo serikali inakosea lakini wao kama wanasiasa wanashindwa kupata nafasi ya kumshauri rais wa nchi.

“Yapo mambo mazito ambayo tungeweza kumshauri rais lakini hajataka kukutana na sisi viongozi wa siasa. Natoa ushauri akutane na sisi kwani kuna mengi ya kumweleza kama vile nchi kuwa na ndege za kumwagilia mashamba badala ya hizo za aibiria na mambo mengine mengi ya kiuchumi,” alisema Rungwe.

Akifafanua zaidi kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa mgombea urais mwaka 2015 alisema, taasisi ya urais inafaa kupewa ushauri ili iwatumie vizuri watu wenye taaluma maana hata Yesu na Mtume Muhammadi walifanikiwa baada ya kuwa na jopo la washauri wao.

Leave A Reply