The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Kama Serikali Mtayumba Katika Hili…. Wanakusini Hatutakubali -Nape

0

MBUNGE wa Mtama, Lindi (CCM), Nape Nnauye ameitaka serikali kuweka misingi thabiti ya utekelezwaji wa ujenzi wa viwanda hapa nchini kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyoeleza.

Nape ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizira ya Viwanda na Biashara iliyowasilishwa na Waziri Mwijage.

“Viwanda ni ukombozi hasa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara lakini ukombozi huu ni vita…. Taarifa tulizonazo ni kwamba kuna makampuni ya nje ambayo hayataki Kiwanda chetu cha Mbolea cha Lindi pale Kilwa kijengwe.”

“Wanapigana kwa ajili ya maslahi yao… kama serikali mtayumba kwa hili, Wanakusini hatutakubali…”

“Vita hii ya wakubwa isituumize sisi, wakapiganie nje ya Lindi lakini sisi tunataka kiwanda chetu.” Alisema Npe.

Leave A Reply