VIDEO: Mama Alia Mbele ya Jafo, Kisa Hiki Hapa!


MWANAMAMA mkazi wa Mkuranga Mkoa wa Pwani amemwangukia Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,  kumsaidia katika kutatua mgogoro uliopo baina yake na baadhi ya majirani wanaodaiwa kumuua mwanaye aliyekuwa mwendesha bodaboda.

Mama huyo amesema  kwamba baada ya uchunguzi watuhumiwa walishikiliwa na jeshi la polisi lakini cha kushangaza maamuzi yaliyotoka mahakamani hayakutoa haki kwake, hivyo ameomba waziri huyo kuingilia upya suala hilo.

 

Katika majibu yake waziri Jafo amesema kuwa kwa vile suala hilo lilifika mahakamaani hawezi kuliingilia na hivyo amemwagiza katibu tawala kulifuatilia upya kujua kama kuna mwanya wowote wa rushwa ulitumika.

Amesema taarifa hiyo ikipatikana apewe yeye ili kulifuatilia.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8

⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Toa comment