The House of Favourite Newspapers

Video: Onyango Afungukia Umri Wake, Amtaja Kagere

0

BEKI mpya wa Simba, Joash Onyango amefungukia kuhusu umri wake kutokana na baadhi ya mashabiki na wadau kuwa na shaka kutokana na muonekano wake kuwa kama ni mwenye umri mkubwa.Beki huyo amesema kuwa anashangazwa na wanaosema yeye ni mzee kwani kama vile anajua umri wake.

 

Onyango ambaye ni beki wa kati aliyekuwa akiichezea Gor Mahia ya Kenya alipata nafasi ya kujiunga na Simba SC baada ya mkataba wake kumalizika katika timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Kenya.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa,mchezaji huyo alisema: “Suala la uzee sijui linapotoka, labda ni baada ya kuweka rangi kwenye nywele na kila mtu ana maoni yake na umri wangu ni kama wanavyoufahamu.

 

”Aidha, Onyango aliongeza kuwa sababu kubwa ya kuondoka katika kikosi cha Gor Mahia ni kuweza kupata changamoto mpya katika maisha ya soka.

 

“Niliipenda Simba tangu nilivyokuwa Gor Mahia kwani Simba ni timu kubwa Tanzania, nimefurahi kukutana na wachezaji niliokuwa nao kule Kenya, pia nimekuja ili niweze kupata changamoto mpya,” alisema Onyango.

Leen Essau,Dar es Salaam

Leave A Reply