The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Samia Awaapisha Viongozi Wateule Ikulu Dar

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha, Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu – Dar es salaam. Leo, 24 Oktoba 2021.

Rais Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 24, 2021 amewaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuwataka kufanya kazi kwa kujituma kwakuwa haitakuwa kama vile walivyozoea.

 

Viongozi  walioapishwa ni Pamoja na Waziri  Innocent  Bashungwa (mb) kuwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

Pauline Philipo Gekul, kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Eng. Kundo Andrea Mathew (mb) kuwa naibu waziri wa habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

Pia amewaapisha wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  Jaji Jacob Casthom Mwatebele Mwambengele, kuwa mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi

 

Magdalena Kamugisha Rwebangira, kuwa mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzI na Asina Abdillah Omar, kuwa mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi.

Leave A Reply