The House of Favourite Newspapers

Video: Said Aliyetobolewa Macho na Scorpion Afunguka Mazito

0

 

SAID aliyetobolewa macho na scorpion aeleza namna anavyoendelea , Jambo hili lilitokea mnamo 2016 mwezi wa tisa tar 6 katika mazingira ya buguruni kipindi ambacho bwana Said akitafuta mboga ya nyumbani kama ilivyo kawaida kwa baba wa familia kurudi na chochote kitu baada ya mihangaiko ya siku nzima.

 

Lakini mambo yalikua ndivyo sivyo baada ya jaama mmoja aliyefahamika kwa jina la Scorpion {Salum} kutokea upande wa nyuma na kuonesha sura ya kuitaji msaada kwa Said kwani alionekana mchafu na sura ya kipole , hata hivyo alimuita kwa pembeni na ndipo alianza kumchoma visu hadi mara saba na kuchuka vitu vyake vya thamani.

 

Jambo hili limeonekana kua la kitofauti kwa mtazamo wa wengi au hata wanajamii kwani wanabuguruni hawakuweza kumsaidia kwa jambo lolote bali walimshangaa hadi anafanyiwa unyama wote na katili huyo.

 

Kunazo changamoto nyingi anapitia ikiwemo ya kulea familia kwani hapo mwanzo wazazi walikua wanamtegemea kwa kila kitu na hata kwa watoto wake pia . Lakini jambo lingine ni mke wake wa pili aliweza kufanya mambo yasiyo mpendeza bwana Said baada ya kujua hajiwezi ikiwemo kutumia mali zake vibaya, feza na hata kudiliki kutoka usiku na wanaume wengine uku yeye akiachwa ndani kalala

Lakini yote kwa yote anamuachia aliye juu kwani yeye ndo muweza wa kila kitu kwani hata hali anayopitia anaijua.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Leave A Reply