The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Sherehe ya Aina Yake PASAKA Kutikisa Mlima wa Moto

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto, Bishop Dkt. Getrude Lwakatare,  anawakaribisha waumini na wananchi wote katika ibada ya Jumapili ya Pasaka itakayofanyika katika kanisa hilo lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, ili wapokee baraka na kufunguliwa kiroho na kimwili.

 

Akizungumza na Global TV, Dkt Lwakatare amesema kuwa kutakuwa na sherehe kubwa kanisani hapo ambapo, watu watakunywa, kucheza na kufurahi kwa pamoja huku wakiendelea kuimarishwa kiroho na kufurahia ushindi wa mauti wa mwokozi Yesu Kristo.

 

Aidha,  amesema ibada ya Jumapili ya Pasaka itakuwa na nguvu kwani siku hiyo watu watafanyiwa maombi maalum na kupata uponyaji kutoka kwa Nabii wa Kimataifa, Dkt. Lucy Tanasha,  kutoka Kenya.

 

Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi watakuwepo kwa ajili ya kumsifu Mungu kwa matendo yake makuu.

MSIKIE DKT LWAKATARE

Comments are closed.