The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Shuhudia Maajabu ya Daraja la Mungu

0
Daraja la Mungu.

Daraja la Mungu ni miongoni mwa vivutio vya kipekee vya utalii mkoani Mbeya ambapo kila mwaka, maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia huenda kulitembelea na kushuhudia maajabu ya uumbaji wa Mungu.

Zipo simulizi za kusisimua kuhusu daraja hilo, nyingine zikidai kwamba kulikuwa na nyoka mkubwa aliyekuwa akiishi chini ya daraja hilo ambaye alikuwa akizuia rasilimali za nchi, yakiwemo madini yaliyokuwa yakipatikana eneo hilo, yasivushwe kupelekwa ng’ambo ya pili.

Zipo simulizi pia kwamba baba wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishindwa kuvuka kwenye daraja hilo kwa sababu ya uvutano mkubwa kati ya kifimbo chake na nguvu zilizokuwa kwenye daraja hilo.

 

 

INSTALL GLOBAL PUBLISHERS APP sasa usipitwe na matukio
PAKUA HAPA==>GLOBAL PUBLISHERS APP

VIDEO YA TUKIO

Leave A Reply