The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Waziri Ndalichako Apokea Msaada wa Vitabu vya Sayansi Kutoka India

0
Waziri Ndalichako.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amepokea jumla ya vitabu 1,000,030 vya masomo ya Hisabati, Baiolojia, Chemistry na Fizikia kutoka kwa balozi wa India nchini, Sandeep Arya kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.

 

Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada huo, waziri Ndalichako alisema kwa niaba ya serikali anaishukuru India kwa msada iliotoa na ameiomba kuendelea kuifadhili Tanzania katika nyanja ya elimu ambapo ameomba iendelee kuleta walimu hasa wa masomo ya sayansi pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania nchini India.

 

Waziri ndalichako alisema kuwa serikali itavigawa vitabu katika shule zenye uhaba wa vitabu, hasa zile zilizopo kwenye maeneo ambayo si rahisi kukuta maduka ya vitabu, na kuongeza kuwa msaada huo umefika katika muda muafaka kwa sababu hivi karibuni serikali ilisambaza vifaa vya maabara kwa shule za nchi nzima.

 

Waziri Ndalichako amesema rais wa nchi hii, John Pombe Magufuli ni mwanasayansi kama alivyo Ndalichako kwa hiyo msada huo utakuwa motisha nzuri kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.

#Global TV Online, kwa kushirikiana na TBC 1, wanakuletea taarifa ya habari iliyosheheni matukio mbalimbali nchi nzima.

VIDEO: Waziri Ndalichako Apokea Msaada wa Vitabu vya Sayansi Kutoka India

Leave A Reply