The House of Favourite Newspapers

Mkoa wa Dar Kutoa Miguu ya Bandia 200 Kwa Wenye Matatizo

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam wenye matatizo ya kutembea kutokana na ulemavu au kuvunjika miguu, kufika ofisini kwake wiki ijayo Jumatatu na Jumanne ili wapimwe saizi ya viungo vyao hivyo vilivyolemaa au kuvunjika na waweze kupewa miguu maalum ya bandia itakayowawezesha kutembea bila matatizo.

 

Makonda ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam aliposema msaada huo uliotolewa na wahisani na wadau wengine, utawafikia watu 200 wenye matatizo hayo.

 

Aliwataka pia Watanzania wengine wenye uwezo wa kutoa msaada huo, wafanye hivyo ili watoe msaada utakaowawezesha watu wengine wenye matatizo kama hayo wanufaike.

TAZMA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply