The House of Favourite Newspapers

VIDEO ZA NGONO: MAKONDA AAGIZA AMBER RUTTY AJISALIMISHE POLISI HARAKA

WAKATI taharuki ikitanda na maswali magumu yakikosa majibu kuhusu nini kimewapata baadhi ya wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva ambao wamekuwa wakiachia video zao chafu (za ngono na za kimahaba) hadharani wakiwa na wapenzi wao wakifanya yao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa agizo kwa video queen maarufu, Amber Rutty kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi leo kabla ya saa 12 jioni.

Makonda ametoa kauli hiyo leo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kusambaa mitandaoni kwa video ya Ambaer Rutty akiwa uchi wa mnyama tena akifanya tendo la ngono na mwanamme jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Taifa na kinyume na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

 

“WAKATI TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote Cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na Rc Makonda watakupatia ujumbe wako,” amesema Makonda.

Hivi karibuni msanii Wema Sepetu naye video zake zilisambaa akipigana busu na kunyonyana ndimi na mwanamme aliyedai kuwani mumewe mtarajiwa licha ya jana kuomba msamaha kwa TCRA na Wataznia wote.

 

Mbali na hao, Sister Fey naye video zake zilisambaa akiwa na mpenzi wake anayedai ni mumewe wakifanya mahaba jambo ambalo lilimuibua Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, juliana Shonza na kumchukulia hatua ikiwemo kumsweka ndani.

 

Wasanii wengine ambao wamewahi kufanya uchafu huo kusambaza video/picha zao za mahaba au za utupu ni Nandy, Bill Nas, Amber Lulu na wengine.

AMBER RUTTY Amwaga Machozi “Kweli Nililala Nao Wote, Shida Tu”

Comments are closed.