The House of Favourite Newspapers

Vigogo Simba Wapandia Dau Pointi Sita CAF

0

SIMBA SC wakiwa wanashuka uwanjani usiku wa leo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie ya Niger, unaambiwa tayari mabosi wa Simba wakiongozwa na Rais wa Heshima, Mohammed Dewji ‘MO’ wameweka mezani dau la kutosha kuhakikisha mastaa wao wanavuna pointi sita ugenini.


Mchezo huo utaanza saa
1:00 usiku, kwenye Uwanja wa Général Seyni Kountché, Niamey nchini Niger. Mara tu baada ya mchezo huo, Simba wataelekea Morocco kucheza dhidi ya RS Berkane, mechi ikipigwa Februari 27, mwaka huu.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema:
“Niwatoe wasiwasi Wanasimba
juu ya michezo hii miwili ya ugenini, tumefanya kazi ya kutosha kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. “Kwanza benchi la ufundi limepata nafasi ya kuwasoma wapinzani wetu USGNwalipocheza dhidi ya RS Berkane.


“Lakini pia sisi kama uongozi
tumeifanya kazi yetu ipasavyo, kama mnavyojua tayari tulitanguliza mashushushu
wetu kwa ajili ya kukamilisha
maandalizi yote na hilo limekamilika.

 

“Bodi ya Wakurugenzi kwa kushirikiana na Rais wetu wa heshima, MO Dewji kama ilivyo kawaida, imetenga fungu la motisha kwa wachezaji, tunaamini kwa maandalizi tuliyoyafanya tutarudi na ushindi wa kishindo.” Taarifa zinasema kwamba, vigogo hao wa Simba, wametenga dola 100,000 (sawa na Sh 230,677,000) kila Simba ikipata ushindi katika michuano hiyo ya kimataifa msimu huu.

STORI: JOEL THOMAS

EXCLUSIVE: JIMMY KINDOKI AWATANGAZIA KICHAPO MTIBWA, ATAMBA – “CHAMA HAMFIKII FEISAL KWA CHOCHOTE…”

Leave A Reply