The House of Favourite Newspapers

Vijana Kinondoni Wapewa Pikipiki, Bajaji

0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na vikundi vya vijana wakati alipokuwa akiwakabidhi bodaboda na bajaji vilivyotokana na mikopo ya asilimia 10 katika makundi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wa kwanza kushoto, Kaimu Mkurugenzi Kiduma Mageni pamoja na Mratibu wa Mikopo Bi. Leah Momba akifuatilia taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo i
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Kiduma Mageni akizungumza na vijana walionufaika na mikopo ya asilimia 10 inayolewa na Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Bi. Halima Kahema akizungumza na viajana walionufaika na mikopo ya asilimia 10 .
Bodaboda zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  kwa vikundi vya vijana kutokana na fedha za mkopo wa asilimia 10 kwa makundi ya vijana, Wanawake na watu wenyeulemavu.
Bajaji zilizitolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  kwa vikundi vya vijana.

 

 

Manispaa ya Kinondoni leo imekabidhi vyombo vya moto vya  usafiri Bodaboda na Bajaji vyenye thamani ya shilingi milioni 91 kwa vikundi 21 vya vijana  kwa lengo la kuwawezesha  katika kujikwamua kiuchumi.

 

Akikabidhi vyombo hivyo ambavyo ni bodaboda 20 na bajaji sita, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa  uwezeshwaji huo unatokana na fedha za  makusanyo ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa  agizo la Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli la kutenga asilimia 10 ya bajeti ya Halmashauri kila mwaka kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

 

“Rais wetu Dk. Magufuli alielekeza fedha hizi ambazo wanapewa makundi haya, zitolewe bila riba ili kila mmoja awe mnufaika, nitumie fursa hii kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kusimamia maelekezo haya vizuri na leo hii tunaona vijana wetu wakinufaika na mpango huu” amesema Mhe. Chongolo.

 

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu. Kiduma Mageni amesema kuwa Kinondoni ni Halmashauri inayotekeleza kwa vitendo na kwamba inazingatia uwezeshwaji wa vijana katika sekta zote za Uchumi na za kijamii na kufafanua kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2019/ 2020  kiasi cha shilingi Bilioni 3.3 kilitengwa kwa vikundi  vikundi 722.

 

Ameongeza kuwa katika fedha hizo, vikundi 510 tayari vimeshanufaika na mkopo, wakati vingine 212 vikiwa  kwenye mchakato wa mwisho wa kupatiwa fedha hizo na kwamba inaendelea kuhamasisha jamii juu ya uwepo wa asilimia 10 kwa ajili ya kuwezesha na kuinua Wananchi kiuchumi kwa akuzingatia ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015.

Leave A Reply