The House of Favourite Newspapers

Takukuru Yawasimamisha Kazi Waliomkera JPM

0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewasimamisha kazi watumishi tisa waliohusika katika usimamizi na ujenzi wa majengo saba ya ofisi za taasisi hiyo ambayo Rais John Magufuli alieleza kutoridhishwa na gharama za ujenzi wake.

 

Uamuzi huo umetolewa saa 24 baada ya  Magufuli kusema kuwa gharama za ujenzi wa nyumba hizo zilizojengwa katika wilaya saba ni kubwa ikiliganishwa na nyumba zenyewe.

 

Akizundua moja ya nyumba hizo eneo la Chamwino, Dodoma, Magufuli alielezea kutoridhishwa kwake na gharama kubwa zilizotumiwa na TAKUKURU, yaani shilingi bilioni 1 ambayo ni sawa na wastani wa shilingi milioni 143 kwa kila nyumba, kwani majengo yaliyojengwa yana thamani ndogo ikilinganishwa na fedha zinazotajwa kutumika.

 

Rais pia alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. Mbungo kurekebisha dosari alizotaja kuwa zinaikabili taasisi hiyo.

 

Aidha, alionyesha kushangazwa na TAKUKURU kutaka kujenga ofisi ya taasisi hiyo katika Wilaya ya Chato kwa kuwa tayari wilaya hiyo inalo jengo la TAKUKURU alilolikabidhi yeye mwenyewe akiwa Waziri wa Ujenzi.

Leave A Reply