The House of Favourite Newspapers

Vilio Vyatawala MAZISHI YA JACK SIMELA, Shuhuda Asimulia Ilivyoteokea – Video

SIMANZI, vilio na majonzi vimetawala katika viunga vya mji wa Morogoro wakati wa mazishi ya aliyekuwa Msanii wa muziki wa Uswazi Mchiriku, Jackson Simela ‘Dogo Jack’, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari na wenzake watano papo hapo Jumamosi iliyopita maeneo ya Nanenane mkoani Morogoro.

 

Kwenye ajali hiyo iliyotokea jirani na kituo cha Mafuta cha Nanenane Dogo Jack alikuwa na wenzake 6 wakielekea makaburini kumzika ndugu wa msanii huyo aitwaye Elizabeth Kazimoto ndipo walipogongana uso kwa uso na lori aina ya scania.

 

Mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Chopa Ally alisema kwa jinsi alivyoshuhudia ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari dogo alilokuwemo marehemu Dogo Jack.

 

Watu sita waliokuwa kwenye hilo gari dogo walikufa hapohapo huku majeruhi mmoja Abdul akiwa amekimbizwa hospital baada ya kichwa kufunuka na kuvunjika mguu.

VIDEO: TAZAMA SHUHUDA AKISIMULIA

Comments are closed.