The House of Favourite Newspapers

Vioja vya Moto Ndani ya Nyumba, Wanafamilia Waomba ‘Poo’

0

WAMEOMBA ‘POO!’ Hivyo ndivyo unavyoweza kusmea kufuatia familia moja katika Mtaa wa Morembe Musoma mkoani Mara kuomba maridhiano na wanafamilia ambao wana mgogoro nao wa ardhi ili kuepukana na vioja vinavyowatokea ndani ya nyumba yao.

Unaambiwa vioja vya aina mbalimbali vimekuwa vikitokea ndani ya nyumba yao ikiwemo moto ambao haujulikani umetokea wapi umekuwa ukiwaka ndani ya nyumba mara kwa mara na kuuunguza magodogo na vitu vingine vya samani ndani ya nyumba hiyo bila kujua chanzo ambapo vitendo hivyo vimewafanya waamue kulala nje.

 

Kwa niaba ya familia, Justin Damian amesema Majirani wa eneo hilo waliwahi kuwaambia kwamba historia ya eneo walilolinunua na kujenga nyumba yao hiyo lina mgogoro wa muda mrefu, hivyo inaweza kuwa chanzo cha vioja hivyo ambavyo sasa vimesababisha familia kulala nje kwa kuhofia maisha yao.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Morembe, Sony Mwinula amesema eneo hilo lina migogoro mingi ya ardhi kwani kila siku kuna watu wanakwenda ofisini kwake na nyaraka nyingi ambazo yeye hawezi kutatua hivyo amewashauri waende kwenye mamlaka ya kisheria kwa ajili ya kupata suluhu.

Leave A Reply