The House of Favourite Newspapers

Viongozi wa Dini Walilia Demokrasia: “JPM Watu Wamejaa Hofu”- Video

“Nimeona tujaribu kuukaribisha mwaka kwa namna nyingine kwa kuwakaribisha viongozi wa dini tuzungumze mambo mbalimbali na kuwasikiliza ninyi kwani ndio mnaotuongoza kiroho, niliona hii inaweza kuwa nafasi ya kupata ushauri kutoka kwenu.” – Rais Dk. Magufuli.

 

“Ninataka mjisikie mko huru wote na ndio maana imekua ngumu kuchagua nani atuongozee maombi lakini ninajua mbele ya Mungu wote mko sawa. Kwahiyo ndugu zangu ninawashukuru sana najua mneniombea sana,kila mara nilipokuwa nikisema naomba mniombee nimekuwa nikifatilia kweli mmeniombea sana,nawashukuru sana.” – Rais Dk. Magufuli.

 

“Nimekuwa nikifuatilia mahubiri mbalimbali kwenye vyombo vya habari, mpaka yule mchungaji anaitwa nafikiri Denis Mgogo ambaye anasema mwenge mtumie kama ‘opportunity’ kwamba muache kulalamika kama nivyuma vitawabana mpaka mtaitika Abee”. – Rais Dk. Magufuli.

 

“Mimi sijawahi kukaa Ikulu kabla, kwa hiyo sijui lakini inaweza ikawa ndio mara ya kwanza kwa Viongozi wote wa kidini, wengi namna hii kutoka kwa kila dhehebu, huu unaweza kuwa mwanzo mzuri.” – Rais Dk. Magufuli.

 

“Rais tuliyekuwa tunamuomba ni wewe, nimeanza kukuombea tangu ukiwa Waziri wa Ujenzi na leo umekuwa Rais bado nakuombea na tunawaza 2025 baada yako itakuwaje, maana tunahitaji Kiongozi kama wewe.” – Mchungaji Amani Lyimo.

 

“Mheshimiwa Rais Magufuli, suala la Demokrasia ni muhimu, watu wana hofu hata kama huambiwi na watendaji wako, kama kazi baba unapiga kweli wewe waachie wazungumze maana Watanzania hawatachagua maneno bali watachagua kazi, wape uhuru waseme.  – Mchungaji Amani Lyimo.

 

“Mchungaji Lyimo ameshauri ziwekwe sheria ili madhehebu yapungue, mimi nina mawazo tofauti na yeye, ukiangalia baa zipo nyingi hadi wengine wananywea chini ya mti, na pombe imesemwa kwenye vitabu vya dini siyo nzuri kwetu sote, Wakristo na Waislam.”  – Askofu Josephat Gwajima.

 

“Pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar kuna msikiti kwa ajili ya Waislam, nilikuwa naomba pia kujengwe pia Kanisa kwa ajili ya Wakristo kuabudu ili kuleta usawa. Suala la kuabudu ni muhimu sana katika mazingira ya kazi.”  – Askofu Josephat Gwajima.

 

“Umefanya jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia, tumekuja kwa pamoja na kwa upendo kujadili mambo ya mbalimbali ya nchi Mungu atakusaidia sana na kukuinua sana katika utawala wako” – Askofu Josephat Gwajima.

 

“Mh. Rais Magufuli Mungu kakutengeneza kuwa madini bora katika madini, ukiona mtu anawajali sana wanyonge, basi fahamu kwamba huyo ni madini bora, wewe ni madini bora”. – Sheikh – Hassan Said Chizenga.

 

“Kwenye Biblia na Quran imeandikwa kamari ni haramu, lakini hapa TZ saivi Vijana wanacheza kamari kupitia Mitandao ukifungua TV unakuta matangazo, haya Makampuni wao ni hapa kamari tu, matatizo nguvu kazi yetu inacheza kamari.” –Kiongozi wa Dini ya Mabohora.

 

“Changamoto inatokea pale Kanisa linapotaka kujenga hosipitali, Serikali nayo inataka eneohilo hilo, tunafahamu ushirikiano wa Serikali na Taasisi binafsi (PPP) katika masuala ya maendeleo.” – Askofu Mkuu Anglikana Chimeledya.

 

“Maadili yanamomonyoka, wanawake wanavaa lakini wapo uchi, vijana wanavaa lakini nguo zao za ndani zinaonekana. Bibilia inakataza wanawake kuvaa nguo za kiume, wakivaa wanatakiwa kufunika maungo yao, wenzetu Waislam niwapongeze wanalizingatia hili.” – Askofu Boniface Zakaria.

 

“Nchi yoyote ile hata kama ina dini na madhehebu mangapi, isipokuwa na maadili ambayo Mungu anapenda na ameyaelekeza, itakuwa na matatizo, wako dada zetu wanatembea ukimwangalia utadhani hajavaa nguo kabisa.” – Askofu Boniface Zakaria.

 

“Serikalini pia wapo Masekretari wa Waziri Mkuu au wa Rais ukimuona nguo ambayo ameivaa ukienda ofisini unashangaa, tunahitaji angalau tukienda kwenye ofisi ya Waziri Mkuu tuone kuwa tunaingia kwenye ofisi ya heshima.” -Askofu Boniface Zakaria.

 

“Mipango miji ni ya Mungu, mivurugano ni ya shetani, tuwe na mpango mkakati wa muda mrefu mathalani wa miaka 50 katika Miundombinu ili tusiwavunjie vunjie wananchi nyumba zao kila wakati, tuna Wataalam tuliowasomesha kwa nini hili linaendelea? tuliangalie hili.” – Mchungaji Josephat Mwingira.

 

“Suala la Wakuu wa Wilaya kutoa amri ya kuwaweka watu ndani wakiwemo Viongozi wa dini, unamweka Kiongozi ndani hii inanipa shida kidogo, je wanataka tuichukie Serikali yetu? Naomba wakuu hao wasipewe mamlaka hayo, wanaitia aibu Serikali kwa kudhalilisha watu. – Mchungaji Josephat Mwingira.

 

“Mimi nina ushahidi, kule Sengerema Mchungaji wangu aliswekwa ndani na Kanisa likabomolewa, sasa nikajiuliza hii maana yake nini? Wakuu wa Wilaya wana madaraka yaliyopitiliza, wanaitia aibu Serikali.” – Mch. Josephat Mwingira.

 

“Mhe. Rais, samahani kwa kusema umechelewa kidogo kutuita, ninashauri tu kwamba kabla haujazipeleka sera zako, ni vizuri tukae pamoja na kujadili kwa sababu ukiwa peke yako inakuwa vigumu sana.” – Mch. Josephat Mwingira.

 

“Hatuwezi kuwa na viwanda bila ya malighafi za kilimo, kilimo cha umwagiliaji ni changamoto, tafiti zinaonyesha kuwa maji yanaendelea kupungua, Tanzania tuna maji mengi ya mvua, yanatuletea shida tukiweza kuyatumia vizuri yataleta ajira.” Mch. Eliona Kimaro. -KKKT.

 

Comments are closed.