The House of Favourite Newspapers

VIONGOZI WA DINI WATOKA NA AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUMTANGULIZA MUNGU KATIKA MAPAMBANO YA CORONA

0

Viongozi wa Dini kupitia Jumuiya ya Maridhiano Tanzania kwa kauli moja wamempongieza Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa namna alivyomtanguliza Mungu mbele katika Mapambano dhidi ya Corona ambapo pia wamelipongeza Bunge la Tanzania kwa msimamo wao wa Kumpongeza Rais.

Hayo yamezungimzwa June 11 katika kikao cha viongozi hao pamoja na Mkuu Wa Mkoa Wa Dares Salaam Poul Makonda ambapo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni Shekh Wa Mkoa Wa Dares salaam Sheikh Alhad Mussa Salum alisema mbali na kumpongeza Rais kwa kusimama imara kuhakikisha makanisa na Misikiti havifungwi pia wanaunga mkono kwa asilimia mia moja juhudi anazofanya katika kuliletea Taifa Maendeleo.


Nampongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa namna anavyoendesha Mkoa huu jambo linalofanya hali ya amani na utulivu kuwa shwari,

“Tunaomba ushirikiano uendelee hivi hivi ili tuweze kudumisha Amani katika Nchi yetu hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea katika kipindi cha Uchaguzi,”alisema.

Aidha MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuombea Watanzania, kufunguliwa fahamu zao maana wengi wao wamefugwa kifikra.

“Maridhiano yanaanza kwa ngazi ya familia na wanatakiwa kuombeana wao kwa wao,Wamekuja watu wengi maskini lakini sasa hivi wananufaika na kufanikiwa na mkoa wetu wakati wenye mkoa hawanufaiki, na kitu chochote na watu wanatakiwa wafunguliwe fahamu zao.

“Tunamshukuru Mungu Rais Magufuli alifunguliwa fahamu mapema, ikamsaidia kununua ndege na kusimamia uchumi wa nchi yetu, amepambana kwa sababu fikra zake zimefunguliwa”alisema.

 

Leave A Reply