The House of Favourite Newspapers

Viongozi Walivyoungana na Mwakyembe Kuaga Mwili wa Mkewe

0
Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda akimpa pole Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na mkewe, Linah Makyembe.

 

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amejumuika na viongozi, wasanii na mamia ya wakazi wa jiji  la Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe.

Mke wa Waziri Mwakyembe alifariki dunia juzi kwa maradhi ya saratani ya titi.

 

Mweneyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdallah Bulembo (kulia) akimpa pole Dkt. Mwakyembe.

Akitoa salamu kwa niaba ya  serikali leo Jumanne Julai 18, Mama Samia amemtaka Dk Mwakyembe kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Amesema: “Tunafahamu kama umempoteza mtu muhimu sana kwako lakini unatakiwa kuwa mvumilivu na kuendelea kumshukuru Mungu kwa hilo, kwa upande wa Serikali tunatoa pole nyingi.”

 

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwapa pole familia ya mwakyembe.

Pamoja na Makamu wa Rais walikuwepo pia viongozi wastaafu wa Serikali, marais Benjamin Mkapa na Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Pia walikuwapo viongozi waandamizi wa Serikali, mawaziri, wabunge, wanasiasa, viongozi wa michezo, wasanii na wanahabari.

Marehemu Linah Mwakyembe Alivyoagwa Dar

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akimpa pole Mwakyembe.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amempongeza, Dk Mwakyembe kwa kutimiza majukumu yake ya kazi ilhali alikuwa akiuguliwa.

“Licha ya kuuguliwa na mkeo mpenzi, uliendelea na majukumu yako kwa jitihada na uaminifu mkubwa, unastahili pongezi,”amesema.

 

Viongozi wa vyama na serikali wakimpa pole Dkt. Mwakyembe.

 

Akiendesha ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kunduchi, Msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Chediel Lwiza amesisitiza Watanzania kuishi kwa kumtumikia Mungu.

 

Mwakyembe akipokea pole kutoka kwa viongozi wenzake.

 

“Mama Mwakyembe alitoa maisha yake kwa ajili ya kanisa, alishiriki shughuli mbalimbali, alijitoa kwa moyo wake wote, tunapaswa kufuata mfano huo, yeye amemaliza kazi tubaki na ujumbe huo,” amesema.

LIVE: Ibada ya Kuaga Mwili wa Mke wa Mwakyembe, KKKT Kunduchi-Dar

PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY | GPL

Leave A Reply