The House of Favourite Newspapers

Baada ya Profesa Jay Kuoa, Vipi Kuhusu Hawa ‘Wahenga’

0
Joti akiwa na rafiki yake wa kike.

WAHENGA ni neno maarufu kwa sasa, watu mbalimbali wanalitumia wakimaanisha mtu wa zamani ama mkongwe ambapo hata kwenye tasnia yetu ya muziki Bongo, wahenga wapo wengi ambao wameanza na muziki huo, wakauacha na wengine bado wanaendelea nao.

 

Listi ya wahenga kwenye Muziki wa Bongo Fleva ni ndefu, unaweza kuchukua hata kurasa tatu kuwataja hapa ambapo katika usiku wa Jumamosi katika Ukumbi wa Mlimani City ulikuwa ni wa furaha kwa familia ya mhenga mmoja aitwaye Joseph Haule ‘Profesa Jay.’

Ambwene Isaya ‘AY’ akiwa na mwenzake.

Katika usiku huo, Profesa Jay ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi alikuwa anasherehekea pamoja na ndugu, jamaa na marafiki ndoa yake aliyofunga mchana wa siku hiyo kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph lililopo Posta ya Zamani, Dar.

Kitendo cha Profesa Jay kuoa kinamfanya kuingia katika orodha ya wakongwe wachache wa gemu la muziki Bongo ‘wahenga’ ambao wameuaga ukapera. Baadhi ya wahenga hao ni pamoja na  MwanaFA, Snare, Mr. Blue, Luteni Kalama na wengine kibao.

 

 

Hata hivyo huku wahenga hao wakipata heshima ya ndoa, swali ni kuhusu wahenga wenzao ambao wapo kwenye muziki ama sanaa kwa muda mrefu wakiwemo kina A.Y, Sugu, Joti, Fid Q, Dully Sykes, Chege na wengine wengi! Kwamba wataoa lini? Ni ukweli kuwa karibu wasanii hao wote wapo ama wamewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi unaofahamika na wengine wana watoto kabisa.

 

Lakini bado wanakosa ile heshima ya ndoa jambo ambalo ni zuri kwa jamii! Katika sherehe ya Profesa, baadhi ya mashabiki waliohudhuria walisikika wakiwataka kina A.Y na Sugu kumfuata pia Profesa Jay kwa kuoa. Waliwahoji kwamba ni kipi kinawafanya wasioe maana kama ni umri unaruhusu, uwezo wao wa kipato unaruhusu na nafasi za kimaisha! Kwa mfano Sugu ambaye ni mzazi mwenziye na Faiza Ally, ni Mbunge wa Mbeya Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Profesa Jay akiwa na mke wake.

(CHADEMA), lakini pia anamiliki miradi mbalimbali ya kumuingizia kipato! Kipi kinamfanya asioe? Au AY ambaye ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kifedha, Fid Q na hata Dully Sykes ambaye anamiliki studio iitwayo 4.12, na wasanii wengine wengi ambao wapo vizuri, hawana budi kuuaga ukapera.

 

Hata hivyo, yanaweza kuwa maamuzi yao binafsi kuishi na wanawake bila kuwaoa kihalali kanisani, misikitini ama kiutamaduni, lakini ili kuipata heshima stahiki ya ndoa ni vyema wahenga hao wakafuata nyayo za MwanaFA, Mr. Blue na Profesa Jay. Watakuwa wamevuka hatua nyingine kwenye maisha yao ambayo walikuwa hawajafikia na pia uzito wa heshima walizonazo utaongezeka maana tayari watakuwa ni ‘waume za watu’.

MAKALA NA BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA

 

Leave A Reply