The House of Favourite Newspapers

Vita ya Harmo, Vanny Boy iko huku!

0

VITA mpya ya wakali wengine wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ na Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ huku kwenye Mtandao wa YouTube.

 

Mashabiki wa Harmonize au Harmo wamejikuta wakitoleana povu na wale wa Rayvanny au Vanny Boy baada ya wawili hao kulingana idadi ya subscribers (wafuasi) kila mmoja akiwa na milioni 1.64.

 

Tofauti iliyopo kwa sasa kati ya Harmo na Vanny Boy na Harmonize kwenye Mtandao wa YouTube ni jumla ya watazamaji kwenye chaneli zao.

Harmo ametazamwa na watu zaidi ya milioni 373.9 huku Vanny Boy akitazamwa na watu zaidi ya milioni 296.1.

 

Wawili hao wamekuwa wakikimbizana kwenye muziki tangu Harmo alipoondoka kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akimuacha Vanny Boy.

Kila mmoja amekuwa akiachia wimbo mkali ili kumfunika mwenzake hivyo kuibua vita baina ya mashabiki wao.

STORI: NEEMA ADRIAN, DAR

Leave A Reply