The House of Favourite Newspapers

Vita Ya Malipo Kiduchu Haijawahi Kumuacha Modo Salama!

0
Mwanamuziki na Video queen, Lulu Diva.

Na Andrew Carlos | Ijumaa | Makala
AMANDA Swartbooi moja kati ya wauza nyago katika video Afrika akitokea Afrika Kusini. Amanda ametokea kujizolea umaarufu kwa kipindi kifupi cha mwaka jana ambapo ametokea katika video kadhaa Afrika ikiwemo Coolest Kid ya Davido akimshirikisha Nasty C wa Afrika Kusini, Four4 ya JR pamoja na Show Me ya Rich Mavoko akiwa na Harmonize.

Licha ya kufanya poa huko, ameshawahi kukiri kuwa kuuza nyago katika video hizo kunamlipa kwani kumempa mafanikio ya kujisomesha katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA) akiwa mwaka wa pili katika masomo ya biashara. Ukija Bongo wapo wauza nyago katika Video za Kibongo ambao ni ‘visu’ lakini wanaangushwa na malipo kiduchu kutoka kwa wasanii husika kiasi cha kufikia kuangalia kazi nyingine za kufanya huku baadhi wakijiingiza katika muziki.
Amber Lulu
Katika makala haya nimekuchambulia baadhi tu ya wauza nyago (modo)ambao vita hii ya malipo kiduchu haijawahi kuwaacha salama kwani wengine wameamua kuachana na kuuza sura na wengine kujiingiza katika kuimba.
LYINN
Alikuja kwa kasi, akavuma katika Video ya Kwetu ya Rayvanny na baada ya hapo akatokomea. Kutokana na kuitendea haki video hiyo, wengi walimtabiri kama miongoni mwa wauza nyago watakaokuja kuliteka soko. Hajashiriki tena katika kuuza sura kwenye video nyingine hadi sasa huku ikisemekana kukwepa malipo kiduchu kwa kila anayemfuata kufanyanaye kazi.
LULU DIVA
Alianza kuuza sura katika Video ya Naogopa ya Mirror kisha katika Remix ya Burger Movie Selfie ya Belle9 na baada ya hapo aliamua kuachana na suala la kuuza nyago na kujiingiza rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Lulu anasema malipo kiduchu na mastaa wengine wakitaka kumtumia bure katika video zao ndivyo vilivyomkimbiza kwenye kuuza sura na kuamua kuimba ambapo kwa sasa anabamba na Ngoma ya Usimuache.
Hamisa Mobeto

MOBETO
Ni modo ambaye pia muuza nyago katika video za Kibongo. Kutokana na malipo kiduchu katika video hizo kumemfanya kupotea kimyakimya katika orodha wauza sura Bongo. Ameshawahi kukiri kulipwa kiasi kikubwa katika video moja tu (Salome ya Diamond) tangu aingie katika kuuza nyago huku akiwa na kumbukumbu ya kulipwa kiduchu katika Video ya Magubegube ya Barnaba.

Agnes Masogange
MASOGANGE
Naye ni miongoni mwa wauza nyago walioanza kupotea kwenye ramani ya muziki Bongo kisa hazilipi. Alianza kutokea katika Video ya Masogange ya Belle9 na baada ya hapo akaonekana kwenye Video ya Magubegube ya Barnaba iliyotoka 2012. Mara ya mwisho kuonekana katika ulimwengu wa wauza nyago ilikuwa katika Video ya Msambinungwa ya Tunda Man akishirikiana na Ali Kiba iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2014.
Mwanadada Gigy Money.


GIGY
Kama ilivyokuwa kwa Amber,    Gigy naye ni miongoni mwa wauza nyago mcharuko ambao wameweza kuzitendea haki video kibao za mastaa Bongo. Ameshatokea katika Video ya Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego, Too Much ya Darassa, Inde ya Dully Sykes na I Get High ya Godzilla. Suala la kuuza sura kwake kwenye video halichukulii siriazi kwa sasa baada ya kumrudisha nyuma kisa malipo kiduchu. Katika moja ya interview aliyowahi kufanya na Global TV Online, Gigy alilalamika kulipwa malipo kiduchu ya shilingi elfu 20 tu badala ya laki tano walizokuwa wameahidiana na Nay wa Mitego.

ZOU
Licha ya kutangaza kwenye redio moja nchini, suala la kuuza sura katika video za Kibongo halichukulii siriazi kivile kutokana na baadhi ya mastaa kupenda kulipa malipo kiduchu. Anaangalia video na video za kutokelezea. Kuonesha hilo ameshatokelezea kwenye video mbili tu Kidebe ya Dogo Janja na Confidence ya TID Mnyama.

AMBER LULU
Unaweza kusema ni miongoni mwa video queen wanaoongoza kutengeneza video nyingi Bongo. Miongoni mwa video hizo ni Inde ya Dully, Daffa ya Pam D, Bongo Bahati Mbaya ya Young Dee, Too Much ya Darassa na nyingine kibao. Ameshawahi kukiri kufanya video bure na wengine kumdhulumu kiasi ambacho wameahidiana kupewa.

Leave A Reply