The House of Favourite Newspapers

VITA YA MAREKANI VS KOREA, MIKWARA YATIKISA DUNIA

0

MAREKANI VS KOREA

WAKATI kukiwa na vita vya maneno kati ya Korea Kusini na Marekani, mikwara yao inayoambatana na tambo za matumizi makubwa ya silaha za nyukilia, inatikisa dunia ya wapenda amani.

 

Kiongozi kijana wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa akitoa vitisho vya kuishambulia Marekani, hasa katika kisiwa chake cha Guam, huku bilionea mtata, Rais Donald Trump, akisema endapo nchi hiyo inayoungwa mkono na China haitaacha vitisho vyake, itakiona cha moto.

MAREKANI VS KOREA
Kiongozi kijana wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un

Huku Korea Kaskazini ikifanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu yanayoweza kufika Guam, Marekani inasogeza manuwari zake za kivita, zinazoweza kuendesha mapambano katika rasi hiyo ya Korea, ikiwa na nia moja tu, ya kumshikisha adabu kijana huyo jeuri.

 

Kinachofanywa hivi sasa na wataalamu wa kijeshi wa Marekani ni kuangalia jinsi gani itakavyopunguza vifo vya raia wasio na hatia, sambamba na madhara mengine ya kibinadamu, mara tu ‘shughuli’ ya kuiangamiza nchi hiyo itakapoanza.

 

Japan, ambayo nayo huenda itashambuliwa na Korea endapo vita hivyo vitapiganwa, inaiomba China, mshirika wa karibu wa Kim, kutumia ushawishi wake kuepusha mapigano, kwani kwa namna hali inavyokwenda, ‘haitamuacha mtu salama’.

 

Mkurugenzi wa zamani wa Mawasiliano katika Ikulu ya Marekani, Anthony Scaramucci, amesema ingawa bosi wake huyo wa zamani anataka suala hilo limalizike kwa njia ya mazungumzo, lakini pia anayo plan B, yenye nia ya kuiadhibu vilivyo Korea Kaskazini.

MAREKANI VS KOREA
Rais wa Marekani, Donald Trump

“Nadhani Marekani ina suluhisho la jambo hilo, suluhisho la kwanza ambalo mara zote ndilo hutangulia, ni mazungumzo ya kidiplomasia na kama hilo litashindikana, basi Donald Trump ana utatuzi mwingine kama itamlazimu,” alisema.

 

NA: MWANDISHI WETU| RISASI

Leave A Reply