The House of Favourite Newspapers

Vita ya namba Yanga Usipime!

KUMEKUCHA Yanga! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Abdul kudai kuwa vita ya namba msimu ujao itakuwa ni balaa kutokana na usajili wa nguvu uliofanywa na uongozi wa timu hiyo hivi karibuni.

 

Hayo ameyasema baada ya kuvutiwa na uwezo wa wachezaji wote wapya waliosajiliwa na timu hiyo hivi karibuni ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na msimu ujao huko Morogoro.

 

Hii inaonyesha kuwa kutakuwa na vita kubwa ya namba ambayo haijawahi kutokea katika siku za hivi karibuni. Mazoezi hayo ya Yanga yanafanyika katika Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro ambako timu hiyo imepiga kambi yake.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Juma amesema: “Kila mchezaji aliyesajiliwa yupo vizuri, kwa hiyo Wanayanga watulie tu na waendelee kutuunga mkono kwa kila jambo kwani msimu ujao kila
kitu kitakuwa sawa.

 

“Usajili uliofanyika binafsi nimeufurahia, kwani umetufanya tuwe na kikosi kipana na chenye wachezaji mahiri kwa kila idara tena zaidi ya wawili. Hakika msimu ujao utakuwa ni bora kwetu, tofauti na uliopita.

 

“Katika mazoezi ambayo tunaendelea kuyafanya hapa Morogoro, jamaa wanaonyesha uwezo mkubwa jambo ambalo linatufanya na sisi wa zamani tuongeze bidii ili kuhakikisha tunakuwa fiti kwani tusipokuwa makini, tunaweza kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza,” alisema Juma.

Wachezaji hao wapya ambao mpaka sasa wapo katika kambi ya timu hiyo huko Morogoro ni Ally Ally ‘Mpemba’ (KMC), Ally Mtoni ‘Sonso’ (Lipuli), Lamine Moro (Ghana), Mustapha Suleiman (Burundi) pamoja na Abdulaziz Makame (Mafunzo FC).

 

Wengini ni Balama Mapinduzi (Alliance), Issa Bigirimana ‘Walcott’ na Patrick ‘Papy’ Sibomana (Rwanda), Juma Balinya (Uganda), Maybin Kalengo (Zambia) pamoja na Mwalimi Salum (Singida United). Ambao hawajajiunga na timu hiyo ni kipa Farouk Shikhalo (Kenya) pamoja na Sadney Urikhob (Namibia).

Comments are closed.