The House of Favourite Newspapers

Vodacom na Smart Codes watangaza Washindi wa Shindano la ‘Vodacom Digital accelerator Program 2020

0
Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangaza washindi wa mchakato wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator.”

 

Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania Plc na Kampuni ya Smart Codes wanayofuraha ya kutangaza washindi wa tatu wa mchakato wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator.”

Mchakato huu ambayo ilizinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kusaidia vijana chipukizi na wanaoanzisha biashara katika sekta ya teknolojia kuweza kufikia mafanikio na kuwa na biashara zenye kuleta faida. Mchakato huu ulipokea zaidi ya maombi 600 ya vijana chipukizi wenye mawazo yao ya kibunifu katika nyanja za kilimo, teknolojia ya huduma za kifedha (Fintech), habari, Afya, elimu na biashara ya mtandao (E-commerce) ilipoanza. Kwa mwaka mzima uliopita wamepitia mafunzo, semina na kupata misaada mbalimbali.

Timu ya majaji wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator.” ikiongozwa na Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto) Mkurugenzi wa Huduma za Tehama kutoka mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Connie Francis, Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph E. Manirakiza, na Edwin Bruno Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Code.

 

Wakati akitoa tangazo hili, Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Bwana Nguvu Kamando amesema maono ya Kampuni ya Vodacom ni kuifikisha Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, na yataweza kufikiwa kwa kuhamasisha mawazo ya kibiashara yenye msukumo wa kiteknolojia ambayo yataleta mabadiliko endelevu.

“Tumevutiwa na kufurahishwa na wajasiriamali chipukizi wote waliochaguliwa katika mchakato huu ya aina yake pekee ya Vodacom Digital Accelerator. Wote walikuwa na mawazo mazuri ya kutumia teknolojia ya kidijitali kubadilisha namna tunavyofanya biashara zetu lakini pia kutatua changamoto za maendeleo. Hongereni sana vijana wote mlioshiriki na ninawahimiza kuendelea kufikiria kwa namna tofauti na kutumia teknolojia ili kuleta mabadiliko. Kwa hiyo basi kwa heshima kubwa naomba kutangaza wajasiriamali chipukizi watatu walioibuka washindi nikianza na mshindi wa kwanza, wapili na watatu:

1. Smart Class

2. Hashtag pools

3. MYHI and E-DISPENSARY

“Ninatoa shukrani zangu kwa wafanyakazi wote wakiwemo majaji na walimu ambao walitoa muda wao na kufanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba tunafika hatua hii. Ninawashukuru watazamaji ambao wameungana na sisi kupitia mtandao kwa ushiriki wenu katika kuifanya sherehe hizi kuwa za mfano wa ushirikiano katika kuunga mkono uvumbuzi kwa manufaa ya Tanzania,” alihitimisha Bwana Nguvu.

Miongoni mwa wakufunzi wakuu katika mchakato wa Vodacom Digital Accelerator na mmoja kati ya wajasiriamali wa kidijitali waliofanikiwa chini Bwana Edwin Bruno ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya Smart Codes alisema ongezeko la ubunifu linaweza kuleta maendeleo ya haraka kupitia maendeleo ya kiteknolojia nchini.

“Tunatoa shukrani zetu kubwa kwa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kwa kuchukua jukumu kubwa katika kuanzisha maendeleo ya teknolojia Tanzania na zaidi kwa kushirikiana na sisi katika kuhakikisha kwamba tunasaidia vijana chipukizi nchini,” alisema Bruno.

Bruno aliongeza kwamba nchini kuna vijana wengi ambao wana masuluhisho mazuri ya kiteknolojia na ambayo yakifanyiwa kazi yatabadilisha taifa hili, “Kampuni ya Smart Codes kupitia atamizi yetu ya Smart Lab ina matumaini ya kuendelea kuziba pengo kati ya wajasiriamali chipukizi na mashirika makubwa. Vile vile kulea wajasiriamali chipukizi nchini na Afrika kwa ujumla. Ninawasifu wajasiriamali wote chipukizi ambao wanafanya kazi kwa bidii na kuwa sehemu ya programu hii na kuonyesha mabadiliko makubwa na mwisho ninawapongeza sana washindi wa leo,” alifafanua bwana Bruno.

Kampuni iliyo chukua nafasi ya kwanza ya Smart Class, ikiwakilishwa na Bwana Adam Duma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo inayo shugulika na huduma za masomo ya ziada kwa kuunganisha waalimu na wanafunzi mtandaoni, alisema amefurahishwa sana kupata fursa ya kuendeleza wazo lake la kibiashara na anashukuru kampuni za Vodacom na Smart Codes kwa msaada wao wakitalaamu kufanikisha hili.

“Ninashukuru kampuni za Vodacom na Smart Codes kwa fursa kubwa walionipa baada ya safari yetu ndefu. Ninawasii makapuni mengine kuiga mfano huu na kusaidia ukuwaji wa ubunifu nchini ili kukuza biashara changa ambazo zimejikita kutatua changamoto mbalimbali nchini”.

Mchakato wa Vodacom Digital Accelerator umeweka mfano chanya kwa mashirika na makampuni makubwa kushiriki kuhakikisha mawazo ya wabunifu yanafanyiwa kazi na kuleta uhalisia ili kuweza kusaidia jamii. Ni wito kwa wavumbuzi wote, wajasiriamali na wataalamu wa teknolojia kufanya jitihada za namna hii ambazo zitabadilisha jamii ya watanzania kwa kutengeneza masuluhisho yaliyo bora zaidi ambayo yatatatua changamoto zinazoongezeka kila siku za ukosefu wa ajira nchini na kuchangia katika kukua kwa uchumi.

Kuhusu Vodacom Tanzania:

Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi na watoa huduma za kifedha kupita simu za mkononi wanaoongoza. Tunatoa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa wateja na makampuni – ikiwemo sauti, data na ujumbe mfupi, video, cloud hosting, masuluhisho ya simu za mkononi na huduma za kifedha – kwa zaidi ya wateja milioni 14.1. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini , ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

Kwa taarifa zaidi , tafadhali tembelea tovuti: www.vodacom.co.tz

Kuhusu Smart Lab:

Smart Lab ni jukwaa la uvumbuzi ambalo linaunganisha taasisi za kielimu na mashirika kwa dhumuni la kuwezesha utengenezaji wa masuluhisho bora zaidi ambayo yataleta athari katika jamii ya Kiafrika.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea [email protected]

 

 

 

Leave A Reply