The House of Favourite Newspapers

Vodacom Tanzania PLC yasherehekea miaka 20 yazindua maduka mapya Dodoma na Dar es Salaam

0

 

Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Usambazaji, Maduka na Huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, George Lugata (kulia) akielezea uwezo wa simu ya smart kitochi ambayo alikabidhiwa mteja, Jovith Muhandiki aliyezawadiwa kwa kutumia mtandao huo kwa muda wa miaka 20, hii ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka la kampuni hiyo lililopo jengo la Palm Village Mikocheni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa na Msimamizi wa duka la Vodacom lililopo jengo la Palm Village Mikocheni, Atilio Lupala wakikata utepe kuzindua duka hilo jipya la kisasa
Mchumi wa jiji la Dodoma, aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji hilo, Charles Rwaembe (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Vodacom lililoko eneo la Chang’ombe Jijini Dodoma. Wengine katika picha kulia ni Mkuu wa Mauzo Kanda ya kati Vodacom Tanzania PLC ,Grace Chambua na kushoto ni Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania PLC kanda hiyo, Andrew Temu
Mkuu wa Mauzo, Vodacom Tanzania PLC, Kanda ya Kati, Grace Chambua (kulia) akimkabidhi zawadi Eliudy Nghwali kama mteja aliyedumu ndani ya mtandao huo kwa miaka 20
Baadhi ya wakazi wa eneo la Chang’ombe Jijini Dodoma wakiwa nje ya duka jipya la Vodacom wakishuhudia uzinduzi rasmi wa duka hilo jipya

 

 

Leave A Reply