The House of Favourite Newspapers

Vodacom Tanzania Yakabidhi Vifaa kwa Shule ya Wasichana Yatima

0
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

VODACOM  Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Wasichana ya Bethsaida mjini Dar es Salaam ambavyo kampuni ilishinda katika mashindano ya makampuni ya Vodacom duniani.

 

Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema, “Elimu ni msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga maisha bora. Hii ni kweli zaidi kwa Watoto yatima ambao tegemeo lao ni elimu pekee.”

 

Shule ya Wasichana ya Bethsaida ilichaguliwa kupokea msaada huu kwakuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akikata utepe kuzindua rasmi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania kwa shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria, Agapinus Tax , Mkuu wa shule hiyo, Hollness Moshi (wanne kulia), Mlezi wa shule, Michael Machali (kulia) na Mwakilishi wa bodi ya shule, Said Ngonyani (watatu kushoto).

 

 

Mkurugenzi wa Vodacom pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni waliikabidhi shule hiyo viti 100, vitabu Zaidi ya 300 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua. Bipenessis alielezea Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom ilijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa kwa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis(katikati) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa mkuu wa shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, Hollness Moshi (kushoto) ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388. Kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria, Agapinus Tax na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.

 

 

Msaada huu unaendana na malengoya Vodacom Tanzania kuongeza ujumuishwaji katika elimu. Hivi karibuni, kampuni ya Vodacom ilizindua mpango wa kupanua wigo wa mfumo wa E-Fahamu kufikia nchi nzima. E-Fahamu ni huduma inayotoa mawaidha ya elimu yenye viwango vya kimataifa na vyenye kukidhi miongozo ya serikali juu ya elimu.

 

Kuhusu Vodacom Tanzania Foundation

The Vodacom Tanzania Foundation ni sehemu ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC yenye mamlaka ya kutoa huduma za kijamii zikiwa zinawalenga zaidi  wanawake na vijana.

Foundation inajumuisha utoaji wa hisani na kutumia uwezo utokanao na teknolojia kuleta suluhisho kwa mahitaji ya kijamii. Ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, Vodacom Tanzania Foundation imesaidia zaidi ya miradi 120 hadi sasa ikiwa imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 15 kuboresha maisha ya watanzania.

Leave A Reply