The House of Favourite Newspapers

Vodacom Watoa Msaada kwa Waathirika wa Mafuriko ya Rufiji na Kibiti

0

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (wa pili kulia) akipokea msaada wa kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko ya Rufiji na Kibiti wenye thamani ya takribani shilingi 250m uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom Tanzania Annette Kanora (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald na Meneja Mauzo wa eneo hilo Suleiman Amri na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele (kulia). Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa wiki mjini Kibiti.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia Taasisi ya Vodacom Foundation, imetoa msaada wa kibinadamu wenye thamani ya takribani shilingi milioni 250 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika maeneo ya Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ndiye aliyepokea msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom, Annette Kanora akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele na kuwashukuru kwa msaada huo huku akiziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa Vodacom.

 

 

Leave A Reply