The House of Favourite Newspapers

VunaDeile Yashirikiana na Mradi wa BBT Kutoa Hamasa kwa Vijana Kujiajiri Kwenye Kilimo

0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashiri wa VUNADEILE, Naseem Allan (katikati), akizungumza wakati wa  hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi waliojishindia kwenye mchezo wa VUNADEILE. Kulia ni Mratibu  kutoka BBT, Vumilia Zikankura.

KAMPUNI ya Three Oceans Ltd inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashiri wa VUNADEILE imesema itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiajiri.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Three Oceans LTD, Naseem Allan wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wanaopatikana kila siku kwenye droo ikiwemo gari mpya aina ya Toyota IST, pikipiki, tv na simu janja aina ya Samsung na iPhone 15.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd, Naseem Allan (kushoto), akikabidhi zawadi ya bajaji kwa mshindi wa VUNADEILE ambapo kila wiki kunatolewa Bajaj tatu. Wengine pichani kutoka kulia ni Mratibu wa BBT, Vumilia Zikankura pamoja na Meneja wa Leseni ya Michezo kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Lenganivo Maeti. Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa katika kuendesha bahati nasibu hiyo, kampuni hiyo inashirikiana na Mradi wa Kilimo wa Building a Better Tommorow (BBT) ili kuhakikisha wanawawezesha vijana.

BBT ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo yenye lengo kuu la kutoa hamasa kwa vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo biashara ili waweze kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa jumla.

 Kwa upande wake, Mratibu kutoka BBT, Vumilia Zikankura amebainisha kuwa BBT imekuwa ikiwawezesha
vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo biashara kwa kuwawezesha mitaji na masoko huku akiwataka vijana kujitokeza kwenye program ya BBT na VUNADEILE Ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali.

 

Leave A Reply